Habari

DE GEA AZIDI KUNUKIA REAL MADRID KWA PAUNI MILIONI 60

on

Real Madrid iko na matumaini ya kutosha kuwa itamnyakua David De Gea kutoka Manchester United kiangazi hiki ikiwa ni miaka miwili tangu dili la kumsajili lishindikane katika siku ya mwisho ya kufunga dirisha la usajili la kiangazi 2015. 
Ingawa miamba hiyo ya Old Trafford inategemewa kuweka vikwazo kwa kila ofa ya Real Madrid, lakini kocha Jose Mourinho tayari ameanza kuandaa orodha ya makipa watakaoziba nafasi ya De Gea.
Mourinho hataki mvutano wa usajili wa kipa huyo uende hadi dakika za mwisho kama ilivyokuwa mwaka 2015 wakati usajili wa De Gea kwenda Real Madrid kwa dau la pauni milioni 29 kushindikana.
Usajili wa De Gea kwenda Real Madrid ulikuwa uende sambamba na kubadilishana na kipa   Keylor Navas ambaye angetoka Madrid kuhamia United. 
Badala yake De Gea, 26, akasaini mkataba mpya wa miaka minne  Old Trafford lakini sasa Real Madrid wako sehemu nzuri ya kumnunua kwa pauni milioni 60.
Dea Gea alitua Manchester United mwaka 2011 kwa pauni milioni 18.9 kutoka  Atletico Madrid. 

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *