DIAMOND PLATNUMZ ASEMA KWA SASA KOLABO NA WASANII WA NIGERIA SIO DILI TENA

BOSI wa lebo ya Wassafi Classic, Diamond Platnumz amesema hivi sasa upepo wa sanaa umebadilika na wala mashabiki hawashtuki unapoamua kufanya nyimbo na wasanii toka nchini Nigeria, tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Diamond ambaye amezindua manukato ya Chubu Perfume amefanya nyimbo na Yuong Killer ambapo ametetea uamuzi huo kuwa lengo ni kukuza kazi za nyumbani.

“Kitu ambacho watu hawajajua ni kwamba muziki Tanzanisa umekuwa unajibeba wenyewe hivyo hata ukifanya ngoma na wasanii toka Nigeria hakiwi tena kitu kipya na wala mashabiki hawastuki,” alisema Diamond.

“Nime fanya wimbo na Young Killer kwa sababu lengo ni kuuvusha muziki wetu ufike mbali zaidi ya hapa,” aliongeza rapa huyo.


Rapa huyo mwenye mafanikio aliendelea kusisitiza kuwa ni ujinga kuendelea kuamini kuwa wasanii toka Nigeria wapo juu kuliko mastaa wa Tanzania.

No comments