DIEGO COSTA APAGAWA KUKUTANA USO KWA USO NA THIERRY HENRY


Wanaweza kuwa ni mashujaa kutoka vilabu pinzani vya London, lakini heshima kati ya Diego Costa na Thierry Henry ikavuka mipaka ya timu zao.

Mshambuliaji wa Chelsea  Costa akakutana na mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Henry siku ya Alhamisi, Mbrazil huyo raia za Hispania akaonyesha furaha yake kukutana na mmoja wa 'wauaji' wasiosahaulika katika Premier League.

Costa akapiga 'selfe' na Henry na kuitupia picha Instagram kwa kusindikiza na maandishi yaliyosema: "Mchana ulio bora kufanyiwa mahojiano na nyota mashuhuri Thierry Henry" 

No comments