DIEGO COSTA ASEMA ALIJIUNGA NA CHELSEA KWASABABU YA KUMKUBALI MOURINHO


Mshambuliaji wa Chelsea  Diego Costa amefunguka kuwa aliondoka Atletico Madrid na kuchagua kutua Stamford Bridge kwa sababu ya Jose Mourinho.

Costa alikuwa chachu ya Chelsea kutwaa ubingwa 2014/2015 kwa kutupia mipira wavuni na kuwa tishio kwa timu pinzani.

Mshambuliaji huyo amesema anamheshimu sana Mourinho ambaye kesho atakuwa akikiongoza kikosi cha Manchester United kukabiliana na Chelsea ndani ya Old Trafford.


No comments