DOKII: KUCHEZA FILAMU NAFASI YA "MWANAMKE JAMBAZI" INANIWIA VIGUMU

MCHEZA filamu nguli wa kike aliyewahi kujipatia umaarufu mkubwa kwa kuigiza kama Mkenya, “Dokii” amesema kuwa miongoni mwa nafasi ngumu kwake kucheza kwenye muvi kwa sasa ni uhusika wa “dada jambazi”.

“Kikubwa kinachonishinda ni kuigeuza sura yangu hadi kuwa kama jambazi kweli kwa muda wote, inaniwia vigumu sana na wakati mwingine najikuta nikishindwa kabisa kucheza,” amesema Dokii.


Hata hivyo, Dokii amesema kuwa atahakikisha hawaangushi mashabiki wake ambao bado wanamuhitaji, kwa kuendelea kucheza filamu huku akijitahidi kulinda miiko ya imani yake kwa upande wa kidini.

No comments