DSS BAND HAISOMEKI, FERGUSON AREJESHA MPIRA KWA KIPA …ARUDI MASHUJAA BAND


Bendi ya DSS ni kama vile haisomeki na sasa mmoja wa waasisi wake, rapa Ferguson ameamua kurejesha mpira kwa kipa.

Habari za uhakika zilizotua Saluti5, ni kwamba Ferguson ameamua kurejea bendi yake ya zamani Mashujaa Band ambayo ipo mbioni kusukwa upya.

DSS Band ilianzishwa mwishoni mwa mwaka jana chini ya Ferguson, Rogart Hegga na Adolph Mbinga, lakini ‘network’ ikakata  baada ya maonyesho machache.

Hata hivyo Feruguson alipoongea na Saluti5 alisema ni mapema mno kuzungumza lolote juu ya safari yake ya kurejea Mashujaa Band kwa kuwa yeye na bendi hiyo bado wako kwenye meza ya mazungumzo.

No comments