DYANA NYANGE AWASHUKURU MASHABIKI KWA TUZO MBILI ZA "BAE AWARDS 2017" ALIZOTWAA NIGERIA

MSANII wa bongofleva, Dyana Nyange ambaye ameshinda tuzo mbili za BAE Awards 2017 nchini Nigeria ambazo ni Best Vocal Performance Female na Best African Artist amewashukuru mashabiki wake waliompigia kura ili kufanikisha ushindi huo.

“Nawashukuruni nyote mliokesha mkiniombea mkinihamasisha na kunipigia kura katika shindano hili mpaka nimeibuka na tuzo mbili,” alisema staa huyo wa bongofleva upande wa kike.

“Bila sapoti ya mashabiki na vyombo vya habari nisingeweza kufikia mafanikio haya niliyoyapata,”aliongeza nyota huyo.

Staa huyo pia alimshukuru mtayarishaji wa nyimbo zake pamoja na menejimenti yake.

Dyana alimaliza kwa kusema kuwa tuzo aliyoipata sio yake bali ni ya Watanzania wote waliokuwa wamemuunga mkono tangu mwanzo wa shindano hilo.

No comments