EDDO SANGA WA MSONDO NGOMA ATHIBITISHA SASA YUKO FITI JUKWAANI

MWIMBAJI “kiraka” wa Msondo Ngoma Music Band, Eddo Sanga amesema kwamba hivi sasa yuko fiti ambapo ameanza kazi kwa kishindo, baada ya kukaa kitako kwa muda wa zaidi ya miezi miwili akisumbuliwa na maumivu ya mguu.

Akiongea na saluti5, Eddo amesema kuwa, anamshukuru Mungu kwa nafuu aliyoipata na amewaeleza mashabiki wa Msondo kwamba ameibuka na kasi ya hali ya juu ili kufidia pale alipokuwa haonekani jukwaani.

“Nashukuru Mungu nimepata nafuu na sasa nimeanza kupanda jukwaani kama kawaida, ninachoweza kuwaambia mashabiki wetu ni kuwa mchakamchaka wa burudani umeanza upya kwa upande wangu,” amesema.


Ndani ya Msondo Ngoma, Eddo aliyewahi kuwa mchezaji mzuri wa mpira wa miguu, hivi sasa anatamba na kibao chake kipya kinachokwenda kwa jina la “Masimango”.

No comments