Habari

EUROPA LEAGUE: MANCHESTER UNITED YATINGA NUSU FAINALI KWA MBINDE …Rashford aokoa jahazi ‘extra time’

on

Manchester United wamelazimika kwenda hadi dakika 30 za ziada (Extra
time) ili kufuzu hatua ya nusu fainaili ya Europa League.
Hatua hiyo iliwasili baada ya United kulazimishwa sare ya 1-1 na Anderlecht
ya Ubelgiji katika dakika 90 za kawaida, matokeo yaliyolandana na yale ya
mchezo wao wa kwanza uliochezwa wiki iliyopita.
Wakiwa kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Old Trafford, United kama
ilivyokuwa kwenye mchezo wa kwanza, walitangulia kupata bao dakika ya 10
mfungaji akiwa yule yule Henrik Mkhitaryan.
Anderlecht wakasawazisha dakika ya 32 mfungaji akiwa Sofiane Hanni,
matokeo yakabaki hivyo hadi dakika 90 za kawaida zilipomalizika.
Marcus Rashford akawa shujaa kwa Manchester United baada ya kuifungia
timu yake bao la ushindi dakika ya 107.

United ilipata pigo dakika ya 22 baada ya kumpoteza beki wake Marcos
Rojo aliyeumia na nafasi yake kuchukuliwa na Daley Blind.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *