Habari

EVERTON YAIREJESHA MANCHESTER UNITED NAFASI YA SITA

on

Everton imeishusha Manchester United hadi nafasi ya sita kwenye
msimamo wa Ligi Kuu ya England baada ya kuifunga Burnley 3-1.
United inabakia na pointi zake 57 sawa na Everton lakini wanaumizwa na
wastani mdogo wa magoli. Hata hivyo Everton iliyopanda hadi nafasi ya tano
inaweza ikarejea nafasi ya sita iwapo United itashinda au kupata sare dhidi ya
Chelsea kesho mchana.
Magoli ya Everton yalifungwa na Phil Jagielka dakika ya 49,  Ben Mee akajifunga dakika ya 71 huku Romelu
Lukaku akitupia la tatu dakika ya 74 wakati bao pekee la Burnley lilifungwa  Sam Vokes kwa njia ya penalti dakika ya 52.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *