FC PORTO WAITEGA ATLETICO MADRID KWA KUKUMBUKA KUIFUATILIA UPYA SAINI YA NICOLAS GAITAN

KLABU ya Porto ya Ureno imeitega Atletico Madrid na sasa wamerejea azma yao ya kutaka kupata saini ya Nicolas Gaitan.

Taarifa za ndani ya klabu hiyo ya nchini Ureno zinasema kuwa uongozi umetoa ridhaa kwa ajili ya kumsajili kiungo huyo kwa gharama ambayo haikutajwa.

Mpango wa mwaka huu ni kama wanakumbusha kidonda cha mwaka jana ambapo klabu hizo mbili ziliingia vitani kwa kila moja kuhitaji mchezaji wa upande wa pili.

Katika harakati hizo, Porto walikuwa wanamweania Nicolas Gaitan katika usajili wa majira ya kiangazi, lakini sasa wameamua kufanya kweli.


Wakisikiliza tetesi hizo, Porto wameweka mezani dau la pauni mil 29 kwa ajili ya kiungo huyo.

No comments