Licha ya ukumbi wa Palm View Kigogo kukaa ‘kiswazi’ sana na kuonakena kama vile haukidhi mahitaji ya bendi kubwa, lakini FM Academia walitandika show ya kufa mtu ndani ya ukumbi huo jana usiku.

FM walidhihirisha kuwa wameenea kila idara – kuanzia mipini ya magitaa, drum, tumba, waimbaji, marapa hadi wanenguaji.

Watu waliofurika kwenye ukumbi walisuuzika na mchanganyiko mtamu wa nyimbo mpya na zamani za FM Academia.

Bendi hiyo ilianza show saa 3.30 ambapo zilipigwa copy za Kicongo hadi saa 5 kamili ndipo vumbi la nyimbo za FM Academia likaanza kutimka huku wimbo “Hadija” ukifungua rasmi program ya bendi hiyo.
USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac