GABO ZIGAMBA ATOA SOMO LA NDOA KWA VIJANA WA SASA... adai wengi wao wameharibiwa na utandawazi

 
MSANII wa filamu Gabo Zigamba amefunguka kwa kudai kuwa vijana wengi wanashindwa kudumu kwenye maisha ya ndoa kwani kuwa wanashindwa kufuata mafundisho ya wazazi wao.

Mwigizaji huyo ambaye sasa ana miaka 12 kwenye ndoa yake na mkewe Fatma wakiwa na watoto wawili Salha na Athuman amefunguka kwa kudai vijana wengi wameharibiwa na utandawazi.

“Waswahili wanasema asiyefuzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu hii ndiyo sababu kubwa zaidi ya tatizo hili vijana wetu hawapati mafunzo kutoka kwa wazazi tena matokeo yake dunia ndiyo inawafunza.


Dunia si pamoja na huu utandawazi ambao umewachizisha vijana wengi wapo vijana ambao hata ukimwuliza ngariba wake nani hamjui.

No comments