Habari

GARETH BALE KUIKOSA BAYERN MUNICH JUMANNE

on

Real Madrid itakuwa bila nyota wake Gareth Bale katika mchezo mgumu wa robo fainali ya Champions League dhidi ya Bayern Munich Jumanne hii.
Zinedine Zidane amesema Bale hajapona kisawasawa tatizo lake la musuli wa mguu wa kulia na ataukosa mchezo huo wa marudiano utakaochezwa Santiago Bernabeu Stadium.
Mabingwa hao watetezi walitoka nyuma na kuifunga Beyern 2-1 katika mchezo wa kwanza mjini Munich.
“Hatacheza kwasababu hatutaki kuhatarisha hali yake, alisema Zidane. “Anataka kurejea na amekuwa akipambana kujiweka sana. Tunatumai tutamtumia katika mchezo wa dhidi ya Barcelona. Tutaangalia maendeleo yake siku baada ya siku”.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *