Gwiji wa Manchester United Gary Neville amechagua mchezaji wake bora wa mwaka Old Trafford lakini sio Zlatan Ibrahimovic wala Paul Pogba.
Ibrahimovic amekuwa nguzo ya timu katika msimu wake huu wa kwanza ndani ya Premier League na ametoa mchango wa magoli 28 kwa timu yake yanayomuweka kwenye tano bora ya wafungaji wanaoongoza kwa magoli.

Pogba nae licha ya kuanza kwa kusuasua lakini sasa ameanza kuonyesha thamani yake kwa kuliteka eneo la kiungo pamoja na pasi bora za mwisho zilizozaa magoli mengi.

Lakini pamoja na yote hayo, Gary Neville amemchagua beki wa kulia Antonio Valencia kuwa mchezaji wake bora kwa Manchester United.
Antonio Valencia  ndiye mchezaji bora wa United kwa mtazamo wa Gary Neville

USISAHAU KUBONYEZA SUBSCRIBE HAPO
LIKE PAGE YETU YA FACEBOOK Saluti5

Post a Comment

 
Top
Nicolaus Trac