GENEVIEVE NNAJI AGEUKIA UTAYARISHAJI FILAMU

STAA wa filamu nchini Nigeria, Genevieve Nnaji amegeukia fani ya utayarishaji wa sinema, kazi ambayo hakuwahi kuifanya katika maisha yake yote ya sanaa.

Genevieve ameamua kufanya kazi hiyo kwa kuanzia na filamu inayotarajiwa kutoka hivi karibuni, inayoitwa “Lion Heart” ambapo yeye atacheza kama mhusika mkuu.

Hata hivyo, ili kuifanya kazi hiyo kuwa bora zaidi, Genevieve amewashirikisha watayarishaji wakongwe ili kumpa uzoefu, ambao ni pamoja na Pete Edochie na Kalu Ikeadu.


Staa huyo amekuwa na mafanikio makubwa kwenye ulimwengu wa filamu huku ikidaiwa kuwa amefika hapo kutokana na uwepo wa bifu ya muda mrefu kati yake na Omotola Jalade.

No comments