Habari

GENK YA MBWANA SAMATTA YACHAPWA 3-2 NA CELTA VIGO KWENYE EUROPA LEAGUE

on

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta ametoka uwanjani bila bao huku timu yake ya Genk ya Ugiriki ikikubali kichapo cha bao 3-2 kutoka kwa Celta Vigo.
Hata hivyo matokeo hayo si mabaya sana kwa Genk ambayo itahitaji angalau ushindi wa bao 1-0 kwenye mchezo wa marudiano ili kutinga nusu fainali ya Europa League.
Genk  iliyokuwa ugenini, ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 10 kupitia kwa Jean-Paul Boetius, lakini Pione Sisto akachomoa dakika tano baadae.
Iago Aspas akaendelea kuwa kwenye kiwango bora kwa kuifungia Celta Vigo bao la pili dakika ya 18 na kumfikishia mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool jumla ya mabao 22 msimu huu.

John Guidetti akaifungia Celta Vigo goli la tatu dakika ya 38 huku Thomas Buffel akiipa Genk bao la pili dakika ya 67.

CELTA VIGO (4-3-3): Sergio, Mallo, Cabral, Fontas, Jonny, Radoja, Wass (Jozabed, 78), Hernandez, Aspas, Sisto, Guidetti (Beauvue, 66)
GENK (4-3-1-2): Ryan, Brabek, Colley, Boetius (Buffel, 62), Trossard (Schrijvers, 82), Malinovskyi (Heynen, 90+2), Uronen, Pozuelo, Berge, Castagne, Samatta

Matokeo ya mechi zote za Europa League ni kama ifuatavyo:
Ajax 2 – 0 Schalke 04
Anderlecht 1 – 1 Manchester United
Celta Vigo 3 – 2 Genk

Lyon 2 – 1 Besiktas

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *