GIDABUDAY ATHIBITISHA WANARIADHA VIJANA WANAENDELEA VYEMA NA KAMBI SEKONDARI YA FILBETY BAYI

KIKOSI cha timu ya Taifa ya wanawake na wanaume ya vijana chini ya miaka 17 ya riadha, inaendelea na kambi kwa ajili ya kujiandaa na mashindano ya kimataifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Afrika Mashariki yatakayofanyika mwezi ujao jijini Dar es Salaam.

Kikosi hicho chenye wachezaji 23 kilipatikana katika mashindano ya taifa ya vijana yaliyofanyika hivi karibuni kwa kushirikisha mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara.

Katibu mkuu wa chama cha riadha Tanzania (RT) Wilhelm Gidabuday alisema kuwa kikosi hicho kilianza kambi hivi karibuni katika shule ya sekondali ya Filbety Bayi iliyopo Kibaha mkohani Pwani.

Aliwataja vijana waliopo kwa wanaume ni pamoja na Donald Joseph, David Kalaghe, Godhard Marando, Shabani Rashid, Frank Onesmo, Ramadhan Juma, Shomari Mohamed, Mark Boniface, Francis Daniel, Michael Kishibe, Jeshua Elisante na Selemani Hamisi.

Wengine wanawake ni pamoja na Winfrida Makonje, Kelfin Kipil, Elizabeth Matias, Rose Seif, Velonica Paulo, Regina Deogratius, Dorcas Boniface, Ester Martine, Kresensia Charles na Mwana Amin Hassan.

“Hiki ndicho kikosi chetu cha vijana ambao wataiwakilisha na kuipeperusha bendera ya taifa ya Tanzania katika mashindano ya Afrika Mashariki ya vijana chini ya miaka 17 ambao kwa sasa wanaendelea na maandalizi,” alisema Gidabuday.


Mashindano hayo hufanyika kila mwaka kwa kushirikisha nchi mbalimbali ambazo ni wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambapo kwa mwaka huu Tanzania Bara ni wenyeji wa mashindano hayo.

No comments