HAJI MANARA AITAKIA KILA LA KHERI SIMBA SC DHIDI YA AZAM FC

AKIWA amepigwa stop kujihusisha na masuala ya soka kwa muda wa mwaka mmoja, msemaji wa klabu ya Simba, Haji Sunday Manara ameitakia kila la kheri timu hiyo kwenye mchezo wao wa leo dhidi ya Azam FC.

Katika posti yake aliyoitupa kwenye ukurasa wa facebook, Manara amemuomba Mwenyezi Mungu kuibariki timu yake hiyo ambayo leo inawania nafasi ya kucheza Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Mchezo wa leo ni muhimu pia hata kwa wapinzani wao, Azam ambao nao wanaitegemea ngazi ya Simba ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kuvuka kuelekea kwenye michuano hiyo ya Shirikisho.

Kwa mujibu wa posti hiyo ya Manara, langoni kwa wekundu hao leo atakuwa kipa Agyei, Besala Bukungu, Mohammed Shabalala, James Kotei, Juuko Murshid, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Laudit mavugo, Ibrahim ajibu na Mo Ibrahim.


Wakati kwenye benchi la wachezaji wa akiba, Simba watakuwa na kipa Manyika Peter, Vincent, Ndemla, Mwinyi Kazimoto, Luizio, Blagnon, Pastori.

No comments