Habari

HAJI MANARA ASEMA MAPAMBANO YA KUDAI HAKI NDIO KWANZA YANAANZA …atoa shinikizo kubwa kwa TFF

on

Aliyekuwa msemaji wa klabu ya Simba
Haji Manara ambaye amefungiwa na TFF kwa mwaka mmoja pamoja na kupigwa faini ya
milioni 9, amesema mapambano ya kudai haki ndio kwanza yanaanza.
Akiandika kupitia ukurasa wake wa
Instagram jana usiku, Haji amesema hata kaa kimya na kwamba atadai haki yake
bila woga kwa vile yeye si aina ya watu wenye moyo dhaifu.
Hiki ndicho alichoandika Haji Manara kupitia ukurasa wake wa
Instagram:
Namshukuru Mungu kwa sasa masuala
yangu binafsi ya kifamilia nimeyamaliza.
Na naweza sema kitu, kwanza niwape
pole nyie kwa haya yaliyonitokea, mm c mtu ninayeamini uonevu c mtu ninayeweza
kunyamaza nikiona haki inaporwa, c mtu mwenye moyo dhaifu wa kuogopa kukosoa
pale panapopaswa kurekebishwa, na always ntabaki hvyo, Juzi Ijumaa jioni
niliambiwa na ofisi yangu imekuja barua toka TFF, ikiniarifu kuna wito wa
kunitaka nifike Karume kusikiliza mashtaka dhidi yangu jpili ya jana asubuhi,
wakati huo nikiwa zbar kwa masuala yangu ya kifamilia, na ofisi ikaiandikia Tff
barua ya kuomba kusogezwa mbele kwa shauri hili hadi jnne ya kesho kwa kuwa ntakuwa
nipo Dar.
barua iliwafikia na bnafsi
nikaongea na Afred lucas msemaji wao na akanijibu ameipokea yy na imegongwa
muhuri na katibu mkuu wa TFF keshaipata, kumbuka hyo ni jioni ya Ijumaaa ,
Jmosi nikampigia Alfred kuulizia kikao hcho cha kamati kimepangwa
lini,akanijibu jtatu ya leo atanijibu, jana tena mkasikia mliyosikia,ni uharaka
upi ilionao tff wa kushindwa kunipa haki ya kusikilizwa? natural justice nchi
hii haitambuliki!!wahaini na wauaji nao pia husikilizwa,,iweje kwa mtuhumiwa
ambae anapigia kelele haki ya mwajiri wake?
kuna hoja dhaifu inajengwa kuwa
nilipaswa nijibu bnafsi barua ya Tff , hv ningewezaje kuijibu barua wakati
sikuwepo Dar na sikuwa nimeiona na vp klabu yangu isiwe na haki ya kunijibia
barua, wakati leo imepokwa haki ya kutokuwa na msemaji? na hv Tff hawajui kuwa
mm nilikuwa naongea kwa niaba ya ofisi na klabu yangu?
nikija sababu za kunifungia
nimejiuliza ni kaka yangu huyu msemwa aliyekuwa anasoma hii hukumu? nimemuona
kwa Millard Ayo, anasoma hukumu ilio kinyume na hati ya mashtaka, hati yao ina
makosa mengine na hukumu pia nyingine, ni aina ya hukumu katili zaid kwa vwango
vya mpira wetu, ila nawaambia Tff Haji hajawahi kuwa dhaifu wa moyo, anaweza
kuwa dhaifu wa kiwiliwili, lakini nna moyo wa Simba,
ntapambana kwa kiwango cha juu
sana, ntadai haki yangu na ya mwajiri wangu kwa viwango, na ntaziomba kamati
zao zipokee rufaa yangu na kukaa kwa uharaka huu walionifanyia, na nipewe haki
ya kusikilizwa,nisihukumiwe kishabiki wala kwa chuki, na nawahakikishia kikao
kitakachokaa na kikiweza kunithibitishia niliosema c sahihi na nimeyatunga na
yamepotosha, ntakubali adhabu hata ya kufungiwa maisha kujihusisha na mchezo
huu ulionilea na kunisomesha.
Mwisho niwaombe fans wetu watulie
tukisubiri hz barua zao, yangu bnafasi na ya klabu.

Usiku mwema.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *