HAJI MANARA ASEMA SIMBA IMEISHIKA PABAYA TFF

SIMBA ilikuwa ifanye kikao cha waandishi wa habari juzi Jumanne lakini ikahairisha kufanya hivyo kwa kile kinachotajwa kama sababu maalum.

Hata hivyo, Mkuu wa idara ya habari na Mawasiliano wa klabu hiyo, Haji Manara amekaririwa akisema kwamba yeye ndie ambaye amehairisha kikao hicho. 

Manara amesema kwamba anasubiri Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limwandikie barua ya kumfungia kama walivyotangaza lakini pia waandike barua ya kuthibitisha kuwa wameirejeshea Kagera Sugar pointi zao tatu.

“Nimekuja kutoka Zanzibar nimekuta maandalizi ya press conference, lakini nimewashauri wenzangu tuahirishe hadi TFF watupatie barua,” amekaririwa akisema Manara.

Habari zinasema kwamba Simba wanasubiri barua hizo mbili za TFF ilki waweze kuchukua hatua ikiwemo kukata rufaa kwenye mamlaka ya juu.

Manara anakusudia kukata rufaa akipinga kufungiwa kujihusisha na soka kwa mwaka mzima huku akipigwa faini ya sh. mil 9 na yeye mwenyewe akisema kwamba hukumu hiyo ni ya kikatili.

Lakini kwa upande wake, Simba kama klabu imekusudia kupinga kupokwa pointi tatu ambazo zimerejeshwa katika klabu ya Kagera Sugar.

TFF imekiri katika huku yake kwamba mchezaji Mohammed Fakhi alionyeshwa kadi tatu za njano lakini Simba ilikata rufaa yake nje ya muda na ikawa haijalipa ada ya rufaa.


“Simba ni kama wameiweka TFF mahali pabaya, wanachosubiri wao ni barua tu waanze kuchukua hatua na huenda hatua hizo zikaivua nguo TFF na ndio maana unaona barua hizo zinacheleweshwa,” kimesema chanzo hicho.

No comments