HAKUNA 'GANDA LA NDIZI' KWA BARCELONA, YATUPWA NJE NA JUVENTUS


Kama mashabiki wa Barcelona walidhani uwanja wao wa Nou Camp utawapa mtelemko wa kurudisha bao 3-0 walizofungwa na Juventus, basi kwa sasa hawana kingine zaidi ya kuugulia maumivu.

Juventus imefanikiwa kulazimisha sare ya 0-0 na kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.

Licha ya kumiliki mpira kwa kiasi kikubwa sana, lakini Barcelona walikosa kabisa mbinu za kupenya ukuta mgumu wa Juventus.
Si Messi, Neymar wala Suarez walioweza kumpa misukosuko kipa mkongwe Gianluigi Buffon.

Barcelona: Ter Stegen 7, Roberto 8 (Mascherano, 78), Pique 8, Umtiti 7, Alba 7, Busquets 8, Rakitic 6 (Alcacer, 58), Iniesta 8, Neymar 7, Suarez 7, Messi 7


Juventus: Buffon 8, Dani Alves 8, Bonucci 9, Chiellini 9, Alex Sandro 8, Khedira 7, Pjanic 8, Cuadrado 8 (Lemina, 84), Dybala 7 (Barzagli, 75), Mandzukic 7, Higuain 7 (Asamoah, 88)

No comments