Habari

‘HAKUNA WA KUBADILI’ YA MIRIAM LUKINDO SASA GUMZO

on

WIMBO mpya wa nyota wa muziki wa Injili nchini Miriam Lukindo Mauki
‘Hakuna wa kubadili’ umeanza kua gumzo kwenye mitandao ya kijamii na vituo
mbalimbali vya redio.
Akizungumza na Saluti 5, Miriam, alisema, tangu aachie wimbo huo wiki
iliyopita amekua akipokea komenti nyingi kutoka kwa mashabiki wake ambao
walikua wamemmisi kwa muda mrefu kwenye gemu.
Alisema,anashukuru kuona mashabiki wake na wadau wengine wa muziki wa
Injili kwa namna walivyompokea kwa nguvu na kumtaka azidi kukaza buti katika
kumtumikia Mungu kupitia uimbaji.
“Nimefarijika na mapokeo ya wimbo wangu huu kwa kweli sikua
mwenye matarajio kama ungeweza kua gumzo hivi kiasi sasa umeniongezea nguvu ya
kuumiza kichwani nipike kazi nyingine nzuri ili kuutangaza utukufu
Mungu,”alisema Miriam.
Itakumbukwa Miriam ambaye aliwahi kutamba na albamu yake ya ‘Ni
Asubuhi’ alikua nje ya gemu kwa muda mrefu kutokana na kutingwa na majukumu ya
kifamilia.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *