HAMORAPA ANUSURIIKA KUPASULIWA NA CHUPA AKITUMBUIZA MAISHA BASEMENT

USIKU wa Jumamosi iliyopita msanii mwenye kiki nyingi Harmorapa alinusurika kujeruhiwa vibaya na chupa wakati alipokuwa akitumbuiza katika ukumbi wa maisha basement uliopo Kijitonyama katika usiku wa Komela.

Akizungumza na kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio Meneja wa rapa huyo, Irene Sabuka amesema Harmorapa alirushiwa chupa lakini kwa bahati nzuri haikumpata la sivyo yangekuwa yanazungumzwa mengine.


“Kiukweli hili jambo la kusikitisha sana Harmorapa alikuwa stejini anaperfom ila kabla ya kumaliza show alitokea mtu mmoja akaRusha chupa stejini bahati nzuri Harmorapa alikwepa ile chupa laiti asingekwepa au ingemkuta kwa bahati mbaya sasa hivi tungekuwa tunazungumza mengine,”amesema meneja huyo.

No comments