HARMONIZE, RICH MAVOKO WAACHIA WIMBO WA PAMOJA UITWAO "SHOW ME"

MARAPA  wa Bongofleva Harmonize na Rich Mavoko ambao wanafanya kazi chini ya lebo ya Wasafi Class Baby, wameachia wimbo wa pamoja unaojulikana kwa jina la "Show Me."

Kampuni ya Wasafi ambayo inaongozwa na Diamond Platnumz, inaruhusu mashabiki wake kupakua kupitia Wasafi .Com kwa shilingi 300.

Harmonize amekuwa miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri chini ya lebo hiyo huku akiwa na nyimbo kadhaa zinazofanya vizuri hivi sasa zikiwemo "Matatizo" na "Aiyola" ambayo ilimweka kwenye ramani ya muziki wa kizazi kipya.


Chini ya Diamond, kundi hilo limekuwa ghali nchini ukilinganisha na makundi mengine yote, hasa baada ya kuanza kuteka soko la muziki kwa ngazi ya kimataifa.

No comments