HASSAN KABUNDA AFICHUA ALIVYOGOMA KUJIUNGA SIMBA NA KUAMUA KUTUA MWADUI

HASSAN Salum  Kabunda ambaye ni mtoto wa nyota wa zamani wa yanga, Salum Kabunda “Ninja”, amedai kuwa aliwahi kufuatwa mara kadhaa na watu wa Simba ili ajiunge nao lakini akagoma na kuamua kuichezea timu ya Mwadui.

Kabunda ambaye mkataba wake na Mwadui unamalizika mwishoni mwa msimu huu, alisema kwamba hakutaka kufanya maamuzi ya kukurupuka kusaini mkataba wa Simba, lakini pia mama yake alikuwa chach ya yeye kuwagomea wekundu hao wa Msimbazi.

“Mama alichangia mimi kutokwenda Simba, lakini hata mimi pia sikutaka kukurupuka na kuingia mkataba na Simba, niliona Mwadui pananifaa wakati huu,” alisema Kabunda.

“Mkataba wangu unamalizika mwisho wa msimu huu na hakuna timu niliyofanya nayo mazungumzo isipokuwa pia sioni ni kwa jinsi gani klabu yagu ya mwadui inaweza kuniacha,” aliongeza nyota huyo.


Pamoja na hayo, nyota huyo alidai kuwa maamuzi juu yahatima yake baada ya kumalika kwa msimu huu yanategemea na namna ambavyo watakubaliana na uongozi wa klabu yake.

No comments