HASSAN KESSY ASHUKURU MASHABIKI WA YANGA KUMPIGANIA KIKOSI CHA KWANZA

BAADA ya kufanikiwa kupenya kwenye kikosi cha kwanza, beki kisiki wa timu ya Yanga, Hassan Kessy amesema kwamba anashukuru sapoti kubwa aliyopata toka kwa mashabiki wa Yanga ambao walikuwa nae bega kwa bega katika kipindi kigumu alichopitia.

Beki huyo ambaye anaonekana kuelewana zaidi uwanjani na winga Simon Msuva, amekiri uungwana toka kwa mashabiki wa Yanga ambao walikuwa nae bega kwa bega tangu alipoachana na Simba ambao walileta vuta nikuvute wakati wa usajili wake.

“Hakuna asiyefahamu nyakati ngumu ambazo nimepitia kabla ya kuwa hapa, kama si msaada wa kocha na sapoti toka kwa mashabiki, kila kitu kilikuwa ovyo juu yangu,” alisema beki huyo aliyesimama badala ya Juma Abdul kwenye mchezo dhidi ya MC Alger na kuonyesha uwezo wa juu.


“Nashukuru sana mashabiki kwa kuniunga mkono lakini pia kocha amefanya kazi kubwa kunijengea hali ya kujiamini mpaka hapa nilipo,” aliongeza beki huyo.

No comments