HASSAN KESSY ASIFU MAELEWANO MAZURI NA MSUVA MCHEZO WAO DHIDI YA MC ALGER JANA

BEKI wa kulia wa Yanga, Hassan Kessy amesifu maelewano mazuri baina yake na winga Simon Msuva katika mchezo wao na MC Alger uliochezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Saalam jana.

Kessy alionekana kucheza vizuri nafasi yake na huku akionyesha bado ana uwezo, licha ya mashabiki wa mpira kumkejeli kwamba amekwisha kimpira.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo, Kessy amesema maelekezo ya mwalimu ndiyo yamepelekea kuonekana kucheza vizuri pamoja na Msuva.

“Tumepata matokeo mazuri nyumbani, kama hapa tumeshinda nadhani wakati wa marudio tutacheza vizuri zaidi ya hapa ili kupata matokeo,” alisema Kessy.


Mchezaji huyo wa zamani wa Simba SC alisema anawashukuru mashabiki wa Yanga kwa kuendelea kumuunga mkono na wasikate tamaa.

No comments