HATIMAYE JOHN TERRY KUBWAGA MANYANGA CHELSEA


Hatimaye John Terry atamaliza miaka yake 22 ya uhusiano wake na Chelsea baada ya kuweka wazi kuwa ataachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Hata hivyo Terry ameweka bayana kuwa bado hana mpango wa kutundika daluga na kwamba ataendelea kusakata kabumbu sehemu nyingine.

Nahodha huyo aliyeibuliwa na academy ya Chelsea, alianza kukichezea kikosi cha kwanza tangu mwaka 1995 na kushinda mataji makubwa 14 na kucheza mechi 713.No comments