HATIMAYE MOURINHO AMKUMBUKA ROONEY …Rashford aanzia benchi


Kocha Jose Mourinho amemwanzisha Rooney kwenye mchezo Premier League dhidi ya Burnley.

Hii inakuwa ni mara ya pili kwa Rooney kuwa kwenye kikosi kinachoanza tangu sikukuu ya Christmas.

Mourinho amefanya mabadiliko nane kutoka kwenye kikosi kilichocheza na Anderlecht ambapo ni Paul Pogba, Jesse Lingard na Eric Bailly pekee waliofanikiwa kupangwa kwenye kikosi kinachoanza leo. Mshambuliaji kinda Rashford naye anaanzisha benchi.

Man Utd: de Gea, Young, Bailly, Blind, Darmian, Ander Herrera, Fellaini, Pogba, Lingard, Rooney, Martial.
Akiba: Carrick, Rashford, Romero, Mkhitaryan, Shaw, Fosu-Mensah, Tuanzebe.

No comments