HATIMAYE NEWCASTLE YAREJEA PREMIER LEAGUE LAKINI HATMA YA RAFA BENITEZ IPO GIZANIHatimaye kocha Rafa Benitez amefanikiwa kuirejesha Newcastle United katika Premier League  - lakini amekataa kuahidi chochote iwapo ataendelea kuifunidsha timu hiyo msimu ujao au la.

Newcastle imerejea Ligi Kuu baada ya msimu mmoja tu, hii ikiwa ni baada ya kuipa kichapo cha 4-1 klabu ya Presten.

Christian Atsu, Matt Ritchie na Ayoze Perez walifunga magoli hayo yaliyoihakikishia Newcastle kurejea Ligi Kuu mbele ya mashabiki 50,000 waliofurika St James’ Park.


Hata hivyo hatma ya  Benitez haipo wazi baada ya kocha huyo wa zamani wa Liverpool na Chelsea kukutaa kutoa jibu la uhakika pale alipooulizwa ambapo alisema: "Huwezi kujua kwa sasa. Hii ni soka, chochote kinaweza kutokea".


No comments