HATIMAYE SIMBA YAPEWA POINTI ZA MEZANI DHIDI YA KAGERA SUGAR …Yanga kwenda mahakamani?


Kamati ya Saa 72 imeizawadia Simba pointi tatu na mabao matatu mezani kufuatia rufaaa yao dhidi ya Kagera Sugar waliodaiwa kumtumia Mohammed Fakhi huku akiwa ana kadi tatu za njano.

 Mohammed Fakhi alicheza katika mchezo baina ya timu hizo Aprili 2, kwenye uwanja wa Kaitaba, Bukoba ambapo Kagera Sugar iliibuka na ushindi wa bao 2-1.

Ahmed Yahya ambaye ni mwenyekiti wa Bodi ya Ligi, akawaambia  waandishi wa habari usiku huu kwenye uwanja wa Karume, jijini Dar es Salaam kwamba Kamati imejiridhisha kuwa ni kweli Kagera Sugar walifanya kosa hilo.

Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Ligi akasema kikanuni kosa hilo adhabu yake ni kupokonywa ushindi. Hakuna namna nyingine.

Kwa pointi hizo za mezani, Simba sasa inafikisha pointi 61 na kuiacha Yanga yenye pointi 56 kwa tofauti ya pointi 5 huku Yanga akiwa na akiba ya mchezo mmoja mkononi.

Wakati Simba ikilamba ushindi wa mezani, upande wa Yanga kuna tishio la kwenda mahakamani kupinga maamuzi hayo ya kamati ya saa 72.

Kama Yanga watakwenda kweli mahakamani, ipo hatari ya Tanzania kufungiwa na FIFA kwa vile ni kinyume na utaratibu kupeleka mambo ya soka mahakamani.

No comments