HAWA KASOMO AFICHUA SIRI YAKE YA KUJITUMBUKIZA KWENYE MUZIKI... asema Kida Waziri na wimbo wake wa "Mawifi" ndie aliyemvuta

MWIMBAJI aliyeanzia kwenye unenguaji, Hawa Kasomo amefichua kwamba amejiingiza katika muziki baada ya kuvutiwa na mwimbaji wa zamani wa Vijana Jazz Band, Kida Waziri.

Akipiga stori na saluti5, Hawa amesema kuwa alianza kumsikia Kida akiimba katika Vijana Jazz kupitia radio wakati akiwa bado msichana mdogo na kushawishika kufuata nyayo zake.

“Nilikuwa nikisikia wimbo wa Vijana Jazz ambao Kida ameimba, hususan ule wa “Mawifi”, haraka nakimbilia ndani, nafungulia radio na kuanza kucheza ambapo sasa baadae nikawa najifunza pia kupitia nyimbo za bendi nyingine,” amesema Hawa.


Hawa ambaye katika unenguaji alikuwa na ngugu yake, marehemu habiba kasomo, amesema hiyo ni kati ya sababu zilizomfanya aweke nadhiri aliyoitimiza hatimaye, ya kuitumikia bendi ya Vijana Jazz ambayo anadai alijikuta ghafla akiwa na mapenzi nayo.

No comments