HAWA KASOMO MBIONI KUREJEA JUKWAANI KALUNDE BAND

WALE mashabiki wa muziki wa dansi “waliommiss” Hawa Kasomo jukwaani wakae mkao wa kuanza kumshuhudia tena akiwa na bendi yake ya zamani aliyoshiriki kuianzisha, ya Kalunde iliyo chini ya Deo Mwanambilimbi.

Akiongea na saluti5, Hawa amesema kuwa kwa kipindi kirefu sasa amesimama kujihusisha na masuala ya muziki akiwa amejikita zaidi kwenye ujasiriamali.

“Hata hivyo mashabiki wengi wamekuwa wakinipigia simu na wengine ninapokutana nao huniuliza kuhusu mpango wangu wa kurejea tena jukwaani, nawaambia wasihofu kwani muda si mrefu nitaibuka upya,” amesema.

Hawa amesema kuwa, kuna mazungumzo yanayoendelea na Kalunde Band wanaomuhitaji, hivyo wakati wowote kuanzia sasa anaweza akarejea upya kuitumikia bendi hiyo.

No comments