HUYU NDIYO RAIS NYOSHI!!! BISHANA NAE JUKWAANI UONE MOTO WAKE …Redo Mauzo alijaribu akaungua


Rais wa bendi ya FM Academia Nyoshi el Saadat (pichani mwenye kilemba) anatajwa kama mtu mwenye roho ya kutu asiyehofia kuchukua maamuzi magumu popote pale.

Nyoshi hanaga kuremba, ukimchezea anakutoa nishai hapo hapo, ukizungua kazini anakupa makavu bila kujali umuhimu wako au uwezo wako katika bendi.

Tarehe 14 mwezi huu ndani ya ukumbi wa Mango Garden, Kinondoni, Nyoshi alimshusha jukwaani mwimbaji Redo Mauzo (picha ndogo) na kutangaza papo hapo kuwa msanii huyo anasimamishwa kazi kwa wiki mbili.

Unajua sababu? Nyoshi alikuwa akiongea jambo fulani kwenye kipaza sauti na Redo pengine kwa bahati mbaya au kwa kujisahau akawa anaongea jambo lingine kwa muda huo huo kupitia kipaza sauti kingine.

Nyoshi akakereka na kumshusha jukwaani Redo na kumsimamisha kwa wiki mbili huku akisisitiza kuwa wanamuziki wanapaswa kuwa na nidhamu na rais wa bendi.

Je ilikuwa sahihi Nyoshi kuchukua hatua hiyo? Adhabu ya kusimamisha msanii kwa wiki mbili kwa kosa kama hilo ilistahili? Wanajua FM Academia wenyewe.

No comments