Habari

IVO MAPUNDA ATOA MAZITO KWA TIMU YA TAIFA YA SERENGETI BOYS

on

IVO Mapunda
kipa aliyedakia timu zote kubwa nchini zikiwemo Simba, Yanga na Azam, amewataka
nyota wanaounda kikosi cha timu ya taifa ya Vijana “Serengeti Boys” kuacha
kubweteka na matokeo ya kirafiki ambayo wanayapata.
Kipa huyo
mkongwe alisema kuwa Serengeti Boys bado wana kazi kubwa nchini Gabon na
isingekuwa vema kama wataanza kulewa sifa mapema na kusahau jukumu
lililowapeleka.
“Kikosi
kinaonekana kuwa na maendeleo mzuri wa matokeo ya mechi za kirafiki lakini
hiyo isiwe sababu ya kuridhika na mafanikio kiduchu, wanapaswa kujua Gabon kuna
kazi kubwa,” alisema Ivo.
“Watanzania
wote macho yapo kwao ndiyo maana unaweza kuona jinsi ambavyo watu wanajitosa
kuchangia, timu ya Taifa ina uhaba wa Mataji na wao wamepewa dhamana hawapaswi
kuzembea hata kidogo.”

Michuano ya
Africon kwa vijana inatarajia kuanza Mei 14 mwaka huu ambako Serengeti Boys
iliweka kambi nchini Morocco kwa ajili ya kufanya maandalizi na imecheza mechi
ya kirafiki na mwenyeji Gabon na kupata ushindi wa mabao 2-1.

Comments

comments

About Saluti 5

Recommended for you

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *