IVORY BAND KUFANYA 'BIRTHDAY' YA MWAKA MMOJA BAADA YA MWEZI WA RAMADHAN


IVORY Band iliyo chini ya Saleh Kupaza, Rama Pentagon na Omar Kisila, imepanga kufanya onyesho maalum litakaloambatana na sherehe ya bendi hiyo kutimiza mwaka mmoja hapo mwezi Julai mwaka huu.

Kupaza ameitonya saluti5 kuwa bendi yao iliasisiwa mwezi Juni ila wamesogeza mbele  sherehe hizo hadi Julai ili kupisha mwezi mtukufu wa Ramadhan unaotazamiwa kuanzia mwishoni mwa mwezi Mei hadi Juni.

Kupaza amesema kuwa, ukumbi, bendi itakayopamba pamoja na tarehe rasmi ya tukio hilo wataviweka bayana muda si mrefu, baada ya kikao cha uongozi kitakachoketi hivi karibuni. 

Moja ya vivutio vya Ivory Band, ni mwimbaji wa kike Amina Juma (pichani juu) mwenye uwezo wa hali ya juu kiumbaji sambamba na ufundi wa kushambulia na kulimudu jukwaa.

No comments