IVORY BAND YAINGIA STUDIO KUPAKUA KETE YAO YA PILI


MUDA huu Ivory Band iko ndani ya Studio ya Amoroso Sound ikipakua kibao chao kipya kinachokwenda kwa jina la “Shika Moyo”, ambacho ni utunzi wake mwimbaji Rama Pentagone.

Mmoja wa wakurugenzi wa bendi hiyo, Salleh Kupaza ameiambia saluti5  kuwa wimbo unasimulia kisa cha mtu anamtaka mpenzi wake kujiamini kwenye mahaba yao kwani moyoni amejaa yeye peke yake.

“Mara tu baada ya kukamilika kurekodiwa kibao hiki tutakisambaza kwenye vituo mbalimbali vya radio pamoja na mitandao ya kijamii kwa ajili ya utambulisho kwa mashabiki wetu,” amesema Salleh Kupaza.

Tayari hadi sasa Ivory Band ina jumla ya nyimbo sita, nyingine zikiwa ni “Mapungufu Yangu”, “Ahadi ni Deni”, “Sikuwa Hivyo”, “Nakutamani” na “Ganda la Muwa Remix” lakini wimbo huu "Shika Moyo" utakuwa wa pili kurekodiwa na kuachiwa hewani baada ya "Ganda la Muwa Remix".
No comments