JAHAZI MODERN TAARAB YAWAHAKIKISHIA MASHABIKI SHOO IPO KAMA KAWA DAR LIVE LEO USIKUPAMOJA na hali ya manyunyu na mvua ndogondogo iliyopo Dar es Salaam tangu asubuhi leo, uongozi wa Jahazi Modern Taarab umeihakikishia saluti5 kuwa shoo yao ya Dar Live, Mbagala itapigwa kama kawaida na kuwaomba mashabiki kuhudhuria kwa wingi.

Mkurugenzi wa Jahazi Modern, Juma Mbizo amesema kuwa kinachoendelea jioni hii ni kuweka mazingira mazuri ukumbini yatakayowafanya mashabiki kutoathirika na mvua endapo itaendelea kunyesha usiku.


“Kwa bahati nzuri ukumbi wa Dar Live una vifichio vya mvua, hivyo niwahakikishie tu mashabiki wetu kuwa hakuna kitakachoharibika hata kama mvua itaendelea kupiga usiku wa leo,” amesema Mbizo.

No comments