JAHAZI MOEDERN TAARAB WAKO MBEYA PASAKA, MKESHA NI SONGEA …Tunduru, Moro nao hawajasahaulika

Jahazi Modern Taarab itatumbuiza mjini Mbeya siku ya Pasaka – Jumapili April 16 – ndani ya ukumbi wa City Pub.
Kabla ya hapo, Jahazi watafanya onyesho la Ijumaa Kuu ya Pasaka Tunduru katika ukumbi wa Amazon halafu wataelekea Songea kwa onyesho la mkesha wa Pasaka a litakalofanyika Serengeti Bar.
Jumatatu ya Pasaka itawakuta Jahazi katika mji wa Morogoro ambapo watarindika kwenye ukumbi wa Airport Bar.

No comments