JAMBO MOJA USILOLIJUA KUHUSU J4 SUKARI NA MWINJUMA MUUMIN


Inawezekana kabisa wewe na yule, mimi na huyu, tulikuwa hatufahamu kuhusu kitu hiki juu ya waimbaji wawili wa dansi Jumanne Seseme (J4 Sukar) na Mwinjuma Muumin.

Akiongea na kipindi cha Afro TZ cha Radio One Jumatatu usiku, J4 akafichua kuwa Muumin alimsaidia vitu vingi katika muziki ikiwemo rap ambayo wengi walijua ni yake yeye (J4).

J4 akasema Muumin alitunga rap ya “Njegere kwa Ubwabwa” na kumwambia J4 aitumie kwenye wimbo wa “Shamba la Twanga” uliotesa ndani ya Twanga Pepeta mwaka 2013 na 2014.


“Ile rap watu wengi wanadhani ni yangu, lakini ilitungwa na Muumin, akaniambia mdogo wangu tumia hii,” alisema J4 katika kipindi hicho kinachoongozwa na Rajab Zomboko.

Kwasasa J4 anatesa na wimbo wake mpya kabisa "Celebrate" aliomshirikisha malkia wa mipasho Khadija Kopa.

No comments