JAMES RODRIGUEZ ATAKA JEZI No 10 MANCHESTER UNITED


JAMES RODRIGUEZ anataka jezi namba 10 ya Manchester United wakati Wayne Rooney akitarajiwa kuondoka Old Trafford kiangazi hiki. 
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Colombia anahusishwa na safari ya kuondoka Real Madrid kuelekea Manchester United.
The Sun la Uingereza linasema Rodriguez tayari ana makabaliano ya mdomo ya kujiunga na Manchester United na tayari mchumba wake anasaka nyumba England.
Jezi namba 10 Manchester United inavaliwa na Rooney ambaye anaelekea kuachana na klabu hiyo aliyoitumikia kwa miaka 18.

No comments