JAY MOE ATOA LA MOYONI KUHUSU ALIVYOMDHARAU BILL NASS

RAPA Juma Mchopanga "Jay Moe" ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya "nisaidie ku share", amesema licha ya kutamani kufanya kazi na rapa wa wimbo "Sitaki mazoea" Bill Nass lakini hatasahau alivyomdharau kabla ya kusikiliza wala kuona video zake.

Rapa huyo amedai kabla ya kumwona, kusikiliza na kutazama video zake hakuwa akijua uwezo mkubwa alionao rapa huyo hivyo hata alivyotumiwa wimbo wa rapa huyo na meneja wake aliudharau hakuusikiliza hadi walipokutana nchini Afrika Kusini.


“Unajua kuna siku meneja wake Billnass “mchafu” alinitumia wimbo aliniomba niwatumie na wengine lakini mimi sikufanya hivyo nilipowakuta Afrika Kusini na kuwahoji wakaniambia wako kwa ajili ya ya kufanya video ya wimbo walionitumia, nilijisikia vibaya sana na niliona aibu maana  niliona video yake ni kali tofauti na nilivyokuwa nikimdhania,” Jay Moe.

No comments