JINA LA MBWANA SAMATTA LAIGUSA MICHUANO YA UEFA

JINA la Mbwana Samatta limeigusa UEFA baada ya mshambuliaji huyo kuifungia timu yake ya GENK jumla ya mabao 6 katika mechi 5 mfululizo zilizopita hivi karibuni.

UEFA inamchukulia Samatta kuwa mmoja kati ya washambuliaji hatari katika michuano ya Europa baada kuposti swali kwenye akaunti yake ya Twitter kuwa   “Je huyu nae anapaswa kufungwa?”

Samatta ambaye ni Mtanzania wa kwanza kucheza michuano ya Kombe la Europa anatarajia kuwepo uwanjani kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Celta Vigo ya Hispania, mechi ambayo itapingwa Aprili 13, katika uwanja wa Balaidos.

Samatta ambaye ni naodha wa timu ya taifa ya Tanzania, ndiye mchezaji pekee wa Tanzania amewahi kubeba medali ya mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani baada ya kubeba ubingwa wa Afrika akiwa na timu ya TP Mazembe ya nchini Congo DRC.


Kama ilivyo kwa Thomas, aliwataka nyota wa Tanzania kutorizika kucheza Simba na Yanga bali watoke nje ya mipaka ili kucheza soka la kulipwa hata kwa mataifa madogo ikiwemo Afrika Kusini ili kusaka njia ya kwenda Ulaya na kuipaisha timu yetu ya Taifa Stars ambayo imeshinda mechi mbili dhidi ya Botswana na Burundi na kupaa kwenye misimamo ya FIFA hadi nafasi ya 137.

No comments