JOEY BARTON AFUNGIWA MIEZI 18 KWA KUBETI


Joey Barton amefungiwa kucheza soka kwa miezi 18 sambamba na kutojihusisha na mambo yoyote yahusuyo soka kwa muda wote huo.
Kiungo huyo wa Burnley amepigwa jela hiyo ya soka baada ya kukiri kujihusisha na michezo ya kubeti.
Barton mwenye umri wa miaka 34, pia amepigwa faini ya pauni 30,000.   
Burnley imesema mchezaji wake amedhamiria kukata rufaa huku FA ikisema kuwa itotoa ombi kwa FIFA adhabu hiyo kutumika dunia nzima iwapo mchezaji huyo mtukutu ataamua kwenda kucheza soka nje ya England.
Imedaiwa kuwa kati ya  26 Machi 2006 na  13 Mei 2016 Barton alibeti mara 1,200 ambayo ni kinyume na sheria kwa mujibu kanunu E8 ya FA.


No comments