JULIET MGBORUKWE AZAWADIWA BMW NA MPENZIWE SIKU YAKE YA KUZALIWA

NYOTA wa filamu mwenye mvuto nchini Nigeria, Juliet Mgborukwe amezawadiwa gari aina ya BMW na mpenzi wake wakati wa kusherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwake.

Juliet ambaye amerudiana na Chima, waliofunga ndoa mwaka 2011 na kutengana mwaka mmoja baadae, hivi sasa wameripotiwa kurudisha tena penzi lao.

Staa huyo alikabidhiwa gari akiwa anasherehekea kutimiza miaka 30 ya kuzaliwa kwake akiwa na Chima aliyemzawadia gari hilo la kifahari.


Juliet aliamua kuposti picha ya gari hilo kwenye mtandao akielezea namna ambavyo penzi lao limefufuka kwa kasi na kuzika tofauti zao walizokuwa nazo kipindi cha nyuma.

No comments