JUMA KATUNDU WA MSONDO NGOMA ASEMA KIMYA CHAKE KINA MAANA YA MASHINDO MKUBWA

MWIMBAJI nguli wa Msondo Ngoma, Juma Katundu amesema kimya chake cha muda mrefu bila kuachia wimbo kina maana ya mshindo mkubwa atakapoamua kuanza kufanya vitu vyake.

Katundu ambaye ni kati ya waimbaji ‘viraka’ ndani ya bendi hiyo kongwe, ameiambia saluti5 kuwa anafahamu mashabiki wamemiss tungo mpya kutoka kwake, lakini amewaomba kuvuta subira akisema kwamba mambo mazuri hayataki haraka.

“Nipo natafakari namna nitakavyoweza kutoka kwa nguvu itakayowashitua wengi, hivyo mashabiki wangu wasijali kwani mimi nipo kwa ajili yao na naahidi kutowaangusha,” amesema Katundu.


Amesema kuwa, anavyo vibao vingi kichwani ambavyo muda si mrefu atateua cha kukifyatua, ila amedai kwamba kama ilivyo kawaida yake ataachia wimbo ambao anaamini utakuwa ‘wa taifa’.

No comments