JURGEN KLOPP ATENGA OFA YA PAUNI MIL 8 KUINASA SAINI YA NYOTA WA WALES

MAJOGOO wa jiji la London wamekataa ofa ya pauni mil 8 walioitoa Swansea wanaotaka kumsajili nyota wa timu ya taifa ya Wales, Joe Allen.

Allen amejikuta hana namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza cha Jurgen Klopp hatua iliyowashawishi Swansea kutupa ndoano.

Nyota huyo anayeiwakilisha Wales katika michuano ya Euro 2016 ianyoendelea nchini Ufaransa amekuwa katika kiwango kizuri ingawa hatua ya kuachana na Liverpoool ni jambo lisilowezekana kwa sasa.

Wakati Swansea wakiamini wanaweza kumng’oa nyota huyo kinachoonekana kuwa ngumu kwake kuondoka ni kutokanana utaratibu waliojiwekea Anfied wa kuachana na wachezaji walio na mkataba mirefu.

Liverpool wamekuwa na kanuni ya kuachana na wachezajhi wale tu ambao wamebakiza kandalasi ya mwaka mwaka mmoja ili hali joe Allen hayupo katika kundi hilo.

Imebainika kuwa Allen hana raha ndani ya kikosi cha klopp kutokana na kutoaminika kikamilifu katika kikosi cha kwanza haliinbayo mshawishi kutaka kuondoka.

Wakitupilia mbali ofa hiyo ya Swansea Liverpool sasa wameweka dau jipya kwa Allen na kwamba kama kuna timu insayomwania lazima waweke mezani kitita cha zaidi ya pauni mil 10.

Hatua ya Liveelpool kukataaa ofa ya Swansea ni kama inapigwa na baadhi ya wachezaji wenzake wa Wales akiwemo Gareth Bale.


Bale aliwataka Liverpool kukubaliana na ofa hiyo kama njia ya kumpa fursa mpya allen kwenda kutumikia kipaji chake kwani ananafasi kubwa ya kucheza katika kikosi cha kwanza akiwa Swansea.

No comments