JUVENTUS WANOGEWA NA WINGA JUAN CUADRADO WA CHELSEA ANAYEKIPIGA KWA MKOPO

JUVENTUS wanakaribia kumsaini winga anayecheza kwa mkopo wa Chelsea, Juan Cuadrado, 28, katika mkataba wa kudumu wenye thamani ya pauni mil. 21.4.

Juan Cuadrado yupo Juve kwa mkopo wa miaka mitatu na aling'ara Jumanne usiku wakati miamba hiyo ya Italia ikiiadhibu Barcelona 3-0 kwenye robo Champions League. 

Chelsea ilimnunua kutoka Fiorentina kwa pauni milioni 23 chini ya Jose Mourinho mwaka 2015 dirisha la Januari  lakini akashindwa kuonyesha ubora wake huku akipata shida kuozea mazingira ya London. 

No comments