JUVENTUS YAZIVAA LIVERPOOL, MANCHESTER UNITED VITA YA KUMWANIA MLINZI WA VILLAREAL


KLABU ya Juventus ya nchini Italia inapigana vikumbo na baadhi ya klabu zinazomfukuzia mlinzi wa Villareal, Mateo Musacchio raia wa Italia.

Lakini kikosi hicho cha kibibi kizee cha Turin itawalazimu kuweka dau la ziada mezani la pauni mil 24 kwa ajili ya jembe hilo.

Pamoja na hilo, Juve watahitaji kupambana kiume kwa ajili ya mlinzi huyo mwenye umri wa miaka 24, kutokana na upinzani mkubwa kutoka katika timu nyingine zinazomwitaji, wakiwemo Liverpool na Manchester United.

United wanatajwa katika dili la kumfukuzia beki huyo wa upande wa kulia kwa ajili ya kuimarisha kikosi cha mashetani wekundu hao.

Lakini taarifa zinasema kuwa Juve wamo katika hatua nzuri ya mazungumzo ya awali na mchezaji huyo kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao kinachopambana kwa ajili ya ubingwa wa msimu huu.


Awali, Liverpool wal;iweka mezani dau la pauni mil 15 kwa ajili ya mlinzi huyo, klabu ya Atletico Madrid hawajaweka bayana kuwa dau la kiungo huyo kiasi gani.

No comments